Kazi yangu ina athari chanya kwa Wakenya wengi wa kawaida.
Ufadhili wa nishati jadidifu unaharakisha teknolojia ya kijani ya Kenya
Kenya itaendelea kupanua nishati yake ya jotoardhi, lakini pia inauzisha nje ujuzi kuhusu umeme na nishati ya kijani kwa nchi zingine barani Afrika. Benki ya Uwekezaji ya Ulaya ni mojawapo ya wakimu wakubwa sana wa shughuli za jotoardhi za Kenya, ambapo iliishafanya uwekezaji mwingi mkubwa tangu miaka ya 1980. Hivi karibuni ilifadhili visima zaidi vya maji na mifumo ya kukusanya moshi kule Olkaria mwaka 2017.
Benki pia ilisaidia shamba kubwa la upepo barani Afrika katika sehemu ya joto na kavu kaskazini mwa Kenya karibu na Ziwa Turkana. Ilitiwa saini ya mkopo wa Euro milioni 225 kwa shamba hili la upepo mwaka 2014 na kutoa msukumo mkubwa katika ufadhili na imani kwa mradi wa muongo wa mzima. Umoja wa Ulaya ulichangia Euro milioni 25 kwa mradi kutoka EU-Africa Infrastructure Trust Fund. Eneo hili sasa lina zaidi ya mitambo 300 ya upepo na linasambaza umeme wa kutosha kwa zaidi ya nyumba milioni.
Anna Mwangi, mwanafizikia wa jiografia katika kituo cha Olkaria na mshauri mwenye kazi kwa wanawake vijana katika sekta ya nishati, anaona sekta hii kama njia nzuri kwa wanawake kusonga mbele. Kujumuishwa ni mada kubwa katika jamii na tasnia ya Kenya, anasema, kwani wanawake zaidi kwa sasa wanatetea kutendewa sawa na kazi sawa. Mwangi amefanya kazi karibu ya miaka 15 kwa Kenya Electricity Generating Co., shirika la umeme la serikali. Mitazamo ya kijinsia imebadilika katika wakati huu na bado inaendelea. “Kenya imeongoza si yo tu katika sekta ya nishati,” anasema, “lakini pia katika kuwawezesha wanawake katika nyanja hii na kukumbuka nyenzo za wanawake.”
Lakini mengi zaidi yanahitaji kufanywa. Wanawake bado wanapaswa kufanya kazi kwa bidii mara 10 zaidi ili kutambuliwa katika tasnia yangu,” Mwangi anasema. “Mimi sasa ni mwanamke mwenye uwezo, lakini ninahitaji kuwa tayari pia kuwawezesha wale ambao wanakuja nyuma yangu, ili tushikane mikono. Hawahitaji kwa ulazima kufuata uwayo wangu, lakini tuko hapa kutengeneza njia. ‘’
Kenya kwa kina
- Kilimo ndiyo injini inayoongoza ya uchumi
- Sekta kuu ambazo nchi inataka kuboresha ni usambazaji wa chakula, utengenezaji, nyumba za bei nafuu na huduma za afya
- Inalenga kutumia 100% nishati mbadalaifikapo mwisho wa muongo
- Kiongozi katika nishati ya jotoardhi na huduma za kulipana kwa simu
Uvumbuzi unaohimiza jamii jumuishi
Vert, kampuni ya kusindika maembe iliyo huko Masindi katika Machakos, mwendo wa saa moja kwa gari kutoka Nairobi, ni operesheni inayokua huku ikileta matokeo chanya kwa jamii. Vert ilipokea mkopo kutoka Equity Bank,mkopeshaji ambaye ni mojawapo ya wasaidizi wanaoongoza wa mashamba madogo. Equity Bank ilisaini mkataba wa Euro milioni 25 mwaka 2019 na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na Euro milioni 25 mnamo mwaka wa 2020. Mikataba hii ilijumuisha ruzuku kutoka Umoja wa Ulaya na ilikuwa sehemu ya Kenya Africulture Value Chain Facility. Mpango huu, unaosaidiwa na Umoja wa Ulaya, unayasaidia makampuni kuwa ya kisasa, kuboresha operesheni za wakulima wadogo, kushawisha jamii jumuishi, na kuwasaidia vijana.
Vert inasambaza juisi kutoka wawazalishaji wakubwa kama vile Coca-Cola na inauza aina mbalimbali za matunda yaliyokaushwa. Inashirikiana na zaidi ya mashamba madogo 500, hasa hasa yale ambayo ni ekari chache tu. Ili kuwa kuwa kijani kibichi, inatumia mbegu na maganda ya maembe kutia mafuta katika vyombo vinavyochemsha bya kiwanda, pamoja na paneli za jua ili kupunguza kutegemea umeme wa gridi wa taifa. Kampuni hii inatoa kipaumbele kuajiri wanawake na kufanya kazi pamoja na mashamba yanayoendeshwa na wanawake, kwa sababu moja ya malengo ya wamiliki wake ni kuongeza ujasiriamali wa kike.
“Kenya inaunda mazingira ambayo ni mazuri kwa wanawake kujihusisha zaidi katika uchumi na kuonyesha kile wanachoweza kufanya,” anasema Maina, mkurugenzi mkuu wa Vert.
“Sasa hivi, ni uchumi’
Jackline Musyoka, ambaye ana digrii katika mikrobiolojia na teknolojia ya biolojia, anafanya kama mchambuzi wa maabara katika Vert. Marafiki zake wengi wanatatizika kupata kazi ikiwa si yo lazima kwa sababu ya kutokuwepo kwa usawa, lakini kama matokeo ya uchumi usiotabirika.
“Nina matumaini kwamba mambo yatakuwa bora zaidi hatimaye, lakini wengi wetu tunapata wakati mgumu,” Musyoka anasema, akipumzika kutoka kazi yake ya kukagua mapipa makubwa ya rojo za maembe ambayo hivi punde yatatumwa kwa kiwanda cha Coca-Cola. “Sasa hivi, ni uchumi. Inawaletea madhara. Huko nje mambo ni magumu. Kila mtu anapambana.”
Bima bunifu kwa wakulima wadogo
Iraki, profesa wa Chuo cha Nairobi, anasema kwamba mustakabali wa kiuchumi wa Kenya utakuwa bora ikiwa Wakenya wanafanya kwa bidii zaidi ili kutatua matatizo kwa kufikiri kwa msingi wa bara na dunia zima.
“Unapoenda katika nchi nyingine barani Afrika, kama Rwanda au Uganda, anasema,” “unaona jinsi Kenya ilivyo sana mbele ya nchi nyingine.”
Kampuni moja inayojaribu kukua kwa kuwa bunifu zaidi na kutatua baadhi ya matatizo muhimu katika jamii ni Pula, inayotoa bidhaa za bima kwa mashamba madogo. Wamiliki wa mashamba madogo mara nyingi hawana mfumo wa usaidizi na wanapata matatizo pamoja na mvua isiyotabirika, joto na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
“Tunapozungumza kuhusu wakulima wadogo, huwa tunaangalia watu ambao wanalima kwa ajili ya kujikimu ulaji, kupata chakula cha kila siku, na labda kuuza mazao yao ili kuweza kupata kipato cha kutumia kulipa ada za shule au kuendesha siku kwa siku nyumba zao,” anasema Faith Kinuthia, mkurugenzi wa operesheni za shamba katika Pula.
Katika ziara kwenye mashamba madogo katika Kaunti ya Nakuru, takriban masaa manne katika gari kaskazini mwa Nairobi, Kinutia anabainisha kwamba “bima inasaidia kulinda wakulima hawa dhidi ya hatari nyingi, kama ukosefu wa mvua au wadudu na magonjwa. Ikiwa wadudu wanakuja katika shamba na kuharibu mazao, mkulima anamaliza akiwa hana kitu. Ukizungumza na wakulima hawa, bila shaka watakuambia kwamba wanajionea mabadiliko mengi yanayoletwa na madiliko ya tabianchi.”
Jibu la teknolojia ya hali ya juu kwa mabadiliko ya tabianchi
Wakulima wadogo nchini Kenya wanawakilisha mojawapo ya sehemu kubwa zaidi za wafanyakazi. Na kilimo ni chanzo kinachoongoza cha shughuli za kiuchumi, ajira na uchuuzi wa nje. Kilimo kinaajiri zaidi ya 40% ya wananchi, ikiwemo wananchi wa vijijini, na unaunda zaidi ya 30% ya pato la taifa la Kenya.
Pula huwasaidia sehemu ya wananchi hawa kwa hitaji kubwa zaidi kwa:
- kutumia teknolojia kuchunguza uharibifu kwa haraka
- ikitoa zana za kidijitali na huduma za ushauri wa kilomo ili kuboresha mazoezi ya kilimo
- kwa kutumia programu za simu zinazorahishia zaidi maajenti wa shamba wanaofanya kazi kwa karibu na wakulima.
Huduma hizi ni muhimu kwani mabadiliko ya tabianchi yanafanya maisha ya wakulima kuwa tete zaidi.
Bima ya tabianchi
Dominick Wanyoike anaendesha shamba dogo la mahindi katika Kaunti ya Nakuru, eneo linalojumuisha kwa ukubwa wakulima wadogo wanaoishi katika chini ya hekta 5 kila mmoja. Vigezo vya hali ya hewa vinabadilika nchini Kenya, na hili hasa linaumiza sana mashamba madogo, anasema Wanyoike, anayetumia mikono yakemi tupu kutenganisha nafaka kutoka kwa maganda madogo ya mahindi kwenye bustani mbele ya nyumba yake.
“Tuliamua kupata bima baada ya mwaka mmoja wa hivi karibuni tulipokuwa tunatarajia mvua kunyesha kama kawaida lakini hazikuja kamwe,” Wanjoike anasema. “Mavuno halisi yalikuwa machache sana, maisha yetu yalikuwa yakianza kuwa magumu zaidi, na ukame unaoongezeka ulikuwa ukifanya maisha kuwa magumu.”
Pula ilianzisha rasmi bidhaa zake za bima kwa wakulima wadogo nchini Kenya mnamo mwaka 2015 na inapanua kwenda katika nchi nyingine katika ukanda. Kampuni inaongeza bima katika gharama za mbegu na mbolea, au inatoa bima kupitia ruzuku za serikali. Hii inapunguza gharama ya bima kwa wakulima. Wakulima hulipwa ikiwa mavuno yao ni chini ya kiwango fulani.
Pula ilipokea ufadhili kwa kampuni inayofadhili biashara zinazoonyesha matumaini makubwa ya kukua, TLcom’s Africa Fund, ambayo inaangazia kampuni za teknolojia zilizo katika hatua za upanuzi. Benki ya Uwekezaji ya Ulaya ni mwekezaji muhimu katika TLcom. Benki hii ilisaidini uwekezaji wa Euro milioni 10 mnamo 2016, na inawazia uwekezaji mwingine kusaidia zaidi ya biashara mpya za barani Afrika. Uwekezaji huu ni sehemu ya kituo cha Boost Africa kinachofadhiliwa na Tume ya Ulaya.
“Ni muhimu kwamba tunaendelea kuendeleza uhusiano wa kutegemeana na wakulima wadogo na kuwatunza, kuhakikisha wako katika biashara,” anasema Kinuthia, meneja wa Pula. “Hii itasaidia kubakisha kila mtu katika biashara. Hatimaye, kilimo ni uti wa mgongo nchini Kenya."
Mabadiliko ya usafiri yanayovutia nchini Kenya
Mabadiliko ya tabianchi, ambayo yana athari mbaya kwa wakulima, pia ni sababu kubwa katika fikra nyuma ya mradi bendera wa mji — mfumo mpya wa mabasi na njia yake yote ya umeme.
Barabara za Nairobi mara nyingi huwa zinajaa na msongamano wa magari huenda polepole sana kwa nyakati za kilele. Kuna mabasi machache ya mji, hakuna tramu au treni za chini ya ardhi, na huduma ya reli iliyozuiwa, kwa hiyo watu wanachukua magari ndogo au mabasi yanayoitwa matatu, au wanatumia magari yao wenyewe kufikia mahali fulani. Kadiri idadi ya wananchi inavyokua, msongamano, nyakati za kusafiri, kelele na uchafuzi wa hewa vinaongezeka, pia.
“Serikali kiukweli inatazama mbele kuboresha hali ya mabasi,” anasema Joseph Kochalle, injinia wa barabara anayefanya pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Eneo la Mji wa Nairobi “Ni siku ngumu, ngumu kufika nyumbani jijini Nairobi au kupanga safari yako.”
“Mtandao wa usafiri wa mabasi mapya jijini Naironi utasaidia watu wa jijini, uchumi, uchafuzi na msongamano sana, kwa sababu usafiri ni mtafaruku sasa,” anasema, akiketi katika mkahawa katika Kitongoji cha Westlands katikati jijini Nairobi, mita chache tu kutoka mojawapo ya vituo vya mabasi visivyo rasmi vyenye shughuli nyingi zaidi. “Mfumo mpya pia utatoa msukumo kwa maeneo mengine ya miji mikuu ambayo yanakuja pamoja, kama Mombasa na Kisumu,”
Njia tano mpya za mabasi jijini Nairobi zitachukua muda unaosalia wa muongo huu ili kukamilika. Mipango ilianza karibu na mwaka 2014, kwa hiyo wakaazi na maafisa wa usafiri wana hamu ya kuharakisha ujenzi. Kenya inatumai mfumo mpya wa kisasa na njia ya umeme itakuwa mfano wa Afrika kwa usafiri fanisi wa kijani.
‘Hatua kubwa ya kusaidia maisha yangu’
Jioni moja katikati jijini Nairobi, Carolyne Omondi anasimama kwa hadhari kando ya barabara kuu yenye shughuli nyingi, akisubiri kuanza safari yake ndefu kuelekea nyumbani katika makazi yasiyo rasmi ya Kibera baada ya siku iliyojaa kazi. Magari, mikokoteni, malori, na lori za mizigo mizito zinapita karibu na miguu yake, akitafuta basi. Kama waenda kwa mguu wengi, Omondi anasubiri katika foleni ndefu na hali zisizo salama ili kupata usafiri kwenye matatu, kwa mara nyingi ambayo ni ya zamani, yenye misukosuko na isiyo na raha.
“Siyo uzoefu mzuri, hasa ninaporudi kutoka kazini,” anasema Omondi, msaidizi wa mganga wa meno katikati mwa jiji la Naironi, ambaye anaishi huko Olympic Estate, sehemu ya Kibera ambayo iko katika kilomita tisa tu mbali lakini inachukua angalau saa moja kufika kupitia msongamano wa magari na foleni ndefu za mabasi. “Unachoka na unapaswa kupambana ili kupata basi,” anasema. “Watu ni wagomvi sana, usalama si yo bora, kuna wanyakuzi wa mfukoni.”
Omondi anataka angetumia muda mfupi zaidi kusafiri. Ingempa muda zaidi wa kupumzika ili kutekeleza lengo lake la kurudi shuleni ili kuwa daktari wa meno.
“Mabasi na usafiri bora,” anasema, “vingekuwa hatua kubwa ya kusaidia maisha yangu.”