Mradi mkubwa wa upanuzi wa maji huko magharibi mwa Kenya unaleta maji safi na udhibiti wa kisasa wa maji taka kwa watu wanaohitaji msaada zaidi

Muuzaji alipaza sauti “afuataye” na kumuamrisha msichana aliyekuwa akingoja kwenye foleni ndefu ili kununua maji kwa nyumba yake. Phoebe Atieno, mwenye umri wa miaka 16, kwa haraka alichukua vyombo vyake vikubwa vya plastiki na kuanza kujaza. 

“Hiyo itakuwa shilingi 50,” huyo mwanamme alisema, huku akinyoosha mkono wake kuchukua pesa zake. Atieno alilipa na kuchukua kwa haraka mapipa yake mazito na kuanza safari ngumu kurudi nyumbani. Ni vigumu kwa mtu mzima au mtoto  kubeba mitungi miwili inayojaa maji, lakini Atieno pia alichoka baada ya siku ndefu shuleni. Alifika nyumbani baada ya saa moja usiku, masaa matatu baada ya kuanza safari.

>@EIB

Mkaaji wa mojawapo ya makazi yasiyo rasmi huko Kisumu, Kenya, akipata maji kwenye sehemu ya jumuiya ya kukusanya maji.

Desturi hii ya kila siku kwa wanawake na watoto ni ukweli wa maisha ambapo Atieno anaishi, katika moja ya makazi yasiyo rasmi huko Kisumu, jiji kubwa la bandari katika mwambao mkubwa  wa Ziwa Victoria magharibi mwa Kenya. Hakuna mabompa mengi ya maji katika eneo hili. Wakaaji wengi husubiri kila siku wachuuzi wa maji wanaofika katika lori za mafuta au mikokoteni ili kuuza maji. 

Benki ya Uwekezaji ya Ulaya inajaribu kuboresha usambazaji wa maji ya bomba katika eneo zima. Mnamo mwaka 2020, Benki ilitia saini mkopo wa Euro 35 milioni ili kusaidia mradi wa Euro 70 milioni unaoboresha  maji na usafi huko Kisumu . Kazi, ambayo bado inaendelea, inaongeza mabomba zaidi ya maji na kuboresha mtandao wa maji taka katika Ziwa Victoria, kwa sababu maji taka mengi ghafi hutiririka keuelekea kwenye vichochoro kote huko Kisumu. Shirika la Maendeleo la Ufaransa lilitoa Euro 20 milioni kwa ajili ya mradi huo na Tume ya Ulaya ikatoa ruzuku ya Euro 20 milioni.



>@EIB

Mkokoteni unaojaa mapipa ya maji ya kuuza kwa wakazi kwenye makazi yasiyo rasmi huko Kisumu.

Hakuna muda wa kucheza

Kwa wakazi wengi wa Kisumu, hasa wa makazi yasiyo rasmi, kutafuta maji ni sehemu kubwa ya maisha yao. Kupata usambazaji wa mara kwa mara wa maji safi ya kunywa  ambayo ni nafuu siyo rahisi. Wakazi wengi hawapati pesa nyingi na sehemu kubwa yake huenda kwa ajili ya chakula na maji. Hii inaacha nafasi ndogo ya akiba na uwekezaji ili kuboresha maisha yao.

“Sina muda wa kucheza na marafiki zangu baada ya shule ,” Atieno anasema. “Muda wangu mwingi unatumiwa kwenye foleni nikitaka maji na kusaidia nyumbani.”

>@EIB

Lori la maji ambalo kwa kawaida hutumiwa kusafirisha maji kwa maeneo ya makazi karibu na Kisumu.

Siyo wakazi maskini tu wanaopata wakati mgumu ili kupata maji mazuri. Mkazi mwingine, Didi Otieno, anaishi katika eneo tajiri katika Mtaa wa Milimani katika sehemu tajiri ya Kisumu lakini yeye pia ana tatizo la maji. 

“Sehemu yetu ya mtaa haihudumiwi na maji ya bomba,” anasema. “Nina uwezo wa kulipa lakini miundombinu haipo. Kwa kawaida mimi huagiza karibu meli mbili za mafuta kila mwezi ili kupeleka lita 10,000 za maji kwa tangi langu la chini ya ardhi katika ua la nyumba yangu. Kutoka hapo, ninaysukuma kwa matumizi ya nyumba nzima.”

Nyumba ya Otieno pia haijaunganishwa na muundo wa maji taka, kwa hivyo aliweka tangi la maji taka ili kushughulikia maji machafu. Kama kungekuweko mitambo ya kudhibiti maji taka na maji katika eneo hili, yeye na majirani wake wangekuwa tayari zaidi kulipa kwa ajili ya huduma hizo, anasema.

Kazi muhimu ya kimataifa

Serikali ya Kaunti ya Kisumu imekuwa ikijaribu kuwasaidia watu kama Atieno na Atieno. Lengo ni wakazi wote kuwa na maji safi, ya bomba. Kumekuwa na uboreshaji mkubwa ukilinganisha na miaka michache iliyopita, lakini mengi zaidi bado yanahitaji kufanywa.

Changamoto ni pampu kuukuu na chakavu, na vifaa vya kudhibiti maji ambavyo havifanyi  ipasavyo. Kuna mabomba mengi yanayovuja. Hakuna mtandao wa maji taka unaotosha ili kukusanya maji taka kwenye mitambo iliyopo ya kudhibiti maji. Hakuna mtandao wa maji taka unaotosha ili kukusanya maji taka kwenye mitambo iliyopo ya kudhibiti maji. Hii inadhuru ubora wa maji, kwa sababu ziwa hili ndilo chanzo kikuu cha maji kwa jiji.

Ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na usaidizi kutoka mashirika mengine ya kimataifa ni muhimu kwa kazi hii, alisema Chrispine Juma, kaimu mkuu wa zamani wa Lake Victoria South Water Works Development Agency, inayosimamia mradi huu. Imekuwa vigumu kuwavutia wawekezaji katika sekta ya maji nchini Kenya kwani faida zake si za kuvutia, alisema.

Kupunguza Uchafuzi wa Ziwa Victoria

Mradi wa Kisumu utaboresha vifaa vya kudhibiti maji na mabomba kwa eneo hili, pamoja na kuongeza mtambo wa kudhibiti maji machafu na kuweka mitandao ya maji taka ya kuunganisha kaya na mabomba  ya usafi ufaao, na kwa hiyo kupunguza uchafuzi wa Ziwa Victoria, ziwa kubwa zaidi lenye maji safi barani  Afrika.

Awamu ya kwanza ya mradi huu inakaribia kukamilika mnamo 2024, na wakazi wameisha anza kuvuna faida kadhaa. Utoaji na upatikanaji wa maji umeongezeka kutoka 26% kufikia 60%. The goal is 90%, when the project is done. Ni  8% tu ya watu waliounganishwa na mtandao wa maji taka hapo awali. Hiyo inatarajiwa kuongezeka  kufikia 40%. Zaidi ya mitandao 1700 ya maji taka itawekwa ili kusaidia kuhudumia karibu wakazi 600,000 wa Kisumu. Katika makazi yasiyo rasmi, asilimia ya nyumba zenye upatikanaji wa maji safi  inatarajiwa kuongezeka na kufikia 70%.

Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, kama mojawapo ya wawekezaji wakubwa zaidi duniani katika maji na udhibiti wa maji machafu, inawekeza katika miradi kama hiyo ya maji duniani. Mnamo muongo uliopita, mkono wa ufadhili wa EU ulitoa zaidi ya Euro 33 bilioni kwa ajili ya zaidi ya miradi 300 ya maji.

“Hapa barani Afrika, EIB imetoa karibu ya Euro 2 bilioni kwa miradi ya maji na maji machafu katika muongo uliopita katika mikopo na ruzuku,” anasema Caroline Ogutu, mhandisi wa maji katika ofisi ya kanda ya Benki ya Uwekezaji ya Ulaya iliyoko huko Nairobi. “Uzoefu uliopatikana katika kuhusika katika miradi ya maji barani kote umeimarisha usaidizi wa kiufundi wa EIB kwa mradi huu.’’

>@EIB

Jan-Willem Lohr, kushoto, na Caroline Ogutu wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya wakizuru mradi wa maji taka huko Kisumu, Kenya pamoja na Paul Agwanda wa Lake Victoria South Water Works Development Agency, kuria.

Maji safi kwa gharama iliyopunguzwa

Kabla ya miradi ya maji kuanza, Atieno hakuwa na muda mwingi wa kucheza au kupumzika baada ya shule. Alianza kazi yake ya shule mara tu baada ya kufika nyumbani. Karibu saa nne za usiku, angeenda kulala. Lakini leo, Atieno ana muda zaidi wa kuishi kama mtoto yeyote mwingine, akicheza na marafiki zake baada ya shule na kufanya kazi za shuleni mapema ili kuweza kupata usingizi wa kutosha. Eneo lake sasa lina wauzaji wengi wa maji ambao wanatoa ugavi mwingi kwa bei nzuri, pamoja na msaada wa serikali ya eneo hilo. Sehemu nyingi za makazi zina maji ya bomba, pia.

“Eneo letu sasa lina maji safi ya bomba yanayotolewa kwetu kwa gharama zilizopungua,’’ Atieno anasema. “Hii imemaanisha kwamba hatuna tena wasiwasi kuhusu magonjwa ya maji, kwani maji tunayotumia yanadhibitiwa. Maji pia ni ya bei nafuu na hatupaswi kuyagawia. Isitoshe, mama yangu na mimi sasa tuna muda mwingi  zaidi wa kupumzika.”

Atieno anatarajia kukamilika kwa mradi, ambao utamaanisha hata na mabomba mengi zaidi ya maji na ya maji taka katika eneo lake na usambazaji wa maji katika nyumba yake unaopatikana wakati wote. Itamaanisha pia kutolazimika kuruka au kupita kwenye maji machafu yanayotiririka kwenye vichochoro vyembamba ambavyo anatumia ili kuzunguka katika eneo.

Faida za miradi ya maji

Kutatua matatizo ya maji kuna faida nyingi sana, anasema Ogutu, mhandisi wa maji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya.

“Kuboresha muundo wa maji wa Kisumu kutasaidia ukuaji wake wa uchumi, pia,” anasema. “Ugavi ulioboreshwa utapunguza magomjwa yanayosababishwa na maji machafu na gharama za huduma za afya  pamoja na kupunguza kwa ukubwa muda unaotumika kwa kuchota maji, ambayo kwa kawaida hufanywa na wanawake na watoto.”